Breaking News

Mapigano makali yaibuka katika mji wa Mosul nchini Iraq


Vikosi vya serikali vilivyoungana na wakurdi

Mapigano makali yameendelea kati ya vikosi vya serikali vya nchi ya Iraq wakishirikiana na Wakurdi dhidi ya vikosi vya Islamic State kugombea mji wa MOSUL.
Ikiwa ni siku ya tatu tangu kutokea kwa mapigano hayo, tayari vikosi vya serikali na vile vya kikurdi vimesogea kwa karibu katika kambi za wanajeshi wa IS vilivyomo katika mji huo wa MOSUL.
Inaripotiwa kwamba hayo ni mapigano makali kuwahi kutokea tangu mwaka 2003 huku vikosi vya jeshi kutoka nchini Marekani vikiunga mkono juhudi za vikosi vya serikali ya Iraq katika vita dhidi ya vikosi vya Islamic State.
Kamanda wa majeshi ya ardhini nchini IRAQ, Luteni Jenerali RIYADH TAWFIQ ameliambia shirika la habari AFP kwamba pamoja na kupata upinzani kutoka kwa vikosi vya Islamic State lakini wanaamini watafanikiwa katika operasheni yao.

No comments