Breaking News

Profesa Ndalichako aagiza bodi ya mikopo(HESLB) kurejea mfumo wa zamani


Waziri wa Elimu sayansi na Mafunzo ya Ufundi Profesa JOYCE NDALICHAKO


Waziri wa Elimu sayansi na Mafunzo ya Ufundi Profesa JOYCE NDALICHAKO ameiagiza bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kurejesha mfumo wa zamani wa kutoa fedha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
 Akizungumza na TBC Profesa NDALICHAKO amekiri kuwepo kwa mapungufu katika namna ya fedha hizo zinavyotolewa hali inayopelekea wanafunzi kupata fedha kidogo ambazo hazikidhi mahitaji.
 Mapema hii leo wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam walilalamikia mfumo wa ugawaji fedha za chakula na fedha ya machapisho wakisema inatolewa kwa kuangalia mfumo wa asilimia kama ilivyo katika utoaji wa ada.(Means tested)

No comments