Breaking News

Donald Trump asema kwamba anaona dalili za wizi wa kura zitajitokeza ili kumfitini asishinde

Mdahalo wa mwisho wa wagombea urais umefanyika nchini MAREKANI kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu Novemba nane mwaka huu Mgombea Urais wa Marekani kupitia chama cha REPUBLICAN DONALD TRUMP Mgombea wa REPUBLICAN DONALD TRUMP na Mgombea wa DEMOCRATIC HILLARY CLINTON walihojiwa kwa saa moja na nusu kuhusu masuala mbalimbali. Miongoni mwa masuala yaliyoulizwa katika mdahalo huo ni iwapo matokeo yatatangazwa je wagombea hao wapo tayari kuyapokea ambapo TRUMP alishindwa kujibu swali hilo. Mara kadhaa TRUMP amenukuliwa akishutumu kuwa uchaguzi huo hautakuwa wa haki kwakuwa anataarifa kuwa kura zitaibiwa.

No comments