Breaking News

CDA Dodoma Wapewa siku nne za mikakati

Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu JENISTA MHAGAMA amezipa muda wa siku nne mamlaka zinazohusika na usimamizi wa mji mkuu DODOMA kuainisha changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua.

Waziri MHAGAMA ametoa agizo hilo baada ya kikao cha pamoja baina Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu DODOMA-CDA na Halmashauri ya Manispaa DODOMA, kuweka mikakati ya pamoja ya upokeaji wa taasisi mbalimbali za Serikali ili kuhakikisha kuwa mifumo yao ni rafiki kwa serikali kuhamia DODOMA.

Katika hatua nyingine, Waziri MHAGAMA amepokea msaada wa Shilingi Milioni Mbili na Laki Tano kutoka Jumuiya ya Shule ya Fountain Gates ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la Ardhi lililotokea Mkoani KAGERA.



No comments